5K’s |Kujielewa, Kujipenda, Kujithamini, Kujiamini na Kujikubali…

Kujielewa, Kujipenda, Kujithamini, Kujiamini na Kujikubali. Ukiwa na hizo 5K  ni moja ya hatua kubwa ya mafanikio katika kujenga a Strong Personality na utu nafsi wenye ‘Utashi’. Huna haja ya kutambuliwa iwe kwa kutajwa ama kusifiwa bila kujali kama ni sifa mbaya ama nzuri ili kujiona kuwa nawe u mtu kati ya watu. Huna haja ya kila likuhusulo liwe kwa misingi ya kusifiwa, sadikiwa, chelekewa, chekwa na mengine mengi – ili tu kutambua ufanyalo ni msingi na la haja. Huna haja ya kumuegemea mwanadamu mwenzio kwa lolote like lililo kwa misingi ya kukubalika bali tu kwa kujikubali.

Muhimu kuliko yoote, huna haja ya kutafuta Furaha na Amani toka kwa wengine bali utapata hayo ndani yako mweneywe daima!

Advertisements
By ashadii

Kufika kwa kujituma na si kwa kutumia…

Kuna watu hufika walipo kwa Uzalendo, jitihada na kujituma. Ila kuna wale wachache hutamani mahala hapo na njia pekee ya kufika hapo ni kupitia migongo ya waliofika wenyewe bila kutambua hata wakifika hawatakaa sababu waliingilia dirishani na si mlangoni.

By ashadii

Mshukuru Mungu kwa ulipofikia…

Mara ya mwisho lini ulijitafakari na kutafakari maisha yako jinsi yalivyo? Wengi wetu tupo kila siku kumuomba Mungu kwa yale ambayo tunataka katika maisha yetu. Lakini je hivi umetambua hapo ulipo na yale uliyo nayo mengi ama baadhi ni yale uliyo omba miaka kadhaa iliyopita na Mungu kakupatia tayari ila umesha sahau na wala hujakumbuka kumshukuru ila umekazana kuomba mengine? Let us be Grateful first kwa yale ambayo Mungu katujaalia leo na tukumbuke kuna wengine wapo kuomba kupata ulicho nacho wewe leo. Huku tukikazana kuishi na kupanga Mipango yetu bila kusahau kumhusisha Mwenyezi Mungu.

– God is Great!

By ashadii

Kujifanya usivyo ili tu ukubalike…

Kitendo cha kuchagua marafiki na kutaka kujibadilisha kuwa kama wao uliowachagua kwa makusudio ya kupandikiza ile feeling ya ‘Belonging’ na kujiona sawa na marafiki ulio wachagua kwa sababu zozote zile ulizo nazo humaliza kabisa mtu kifikra ya kutambua wewe ni nani… Ukiwa na bahati unaweza kushtuka ukarudi nyuma na kujiachia jinsi ulivyo bila kujifanya… Ili ukipata marafiki upate wale ambao watakuchagua kwa jinsi ulivyo na si jinsi unavyojifanya ulivyo…

By ashadii

Mabaya na Mazuri yapo kwa ajili ya kila mmoja…

Katika maisha kuna yale ambayo hujulikana kama mabaya na mazuri. Mabaya huwa mabaya in the sense kuwa si matarajio ya mtu kukutwa nayo, iwe ugonjwa usiotibika, iwe ni kutendewa ama kutendwa na vile asivyo taraji ama iwe lolote lile ambalo haliwezi mfurahisha likimkuta.

Ajabu ni kuwa pamoja na kuwa sie wote ni wanadamu, na wote tunajua kuna mabaya na mazuri maishani; pale baya linapotukuta, hushangaa na kusononeka huku tunajiuliza ‘Kwa nini mimi?’ Pengine hata tukamlaumu Mungu kwa hilo. Ndio maana kuna umuhimu mwenzio anapopata baya juu yake kuwa na imani ya dhati na ikiwezekana kuwa msaada kwake, sababu mwisho wa siku nawe utahitaji hilo toka kwa wengine ‘baya’ litakapokukuta wewe.

By ashadii

Marafiki wenye urafiki Kafiri…

Kuwa makini na wale waliokuzunguka… Wale wanaodai ni marafiki zako. Kuna wale wachache ambao raha yao ya wewe kuwa katika maisha yao ni sababu wanaona wamekuzidi… Iwe kwa Uzuri, Kipato, Exposure ama lolote lile.

Wao hukuchukulia kama chambo cha yeye kujisikia vizuri kwa kujiona yeye ni bora kuliko wewe. Siku zote yeye hutaka wewe ubaki hapo hapo ulipo na si ubadilike na kuwa na mafanikio ama kuendelea zaidi ya hapo ulipo.

By ashadii

Kufikia Kilele cha Maisha Bora kuna njia nyingi…

Wote tunapenda kuwa juu Kimaisha na kupenda tufike kilele cha maisha Bora; Lakini si wote tuliokuwa na bahati ya kuchagua njia sahihi kutufikisha hapo ambapo tunataka. Pengine tokana na misingi mibovu, ushauri mbovu, walezi wabovu na mengine mengi ya kutufanya tuchemke Ki maisha.

Uzuri wa yoote hayo.. Haijalishi kuwa tumechagua njia ambayo si sahihi ili kufika kilele cha maisha bora. Kinachojalisha ni sie kutambua haraka njia tuliyopo si sahihi na twapaswa kujaribu njia nyingine mara moja hadi pale tutakapofika kilele cha maisha bora tuliyolenga – Bila kujali tutafanikiwa ama lah.

By ashadii