Mfarakano usio MFarakano haja…

Itokeapo mifarakano kati ya wawili ni nadra sana kukuta mhusika wa pande zote mbili kusema ukweli na kutambua nafasi yake katika mfarakano huo, bila kujalisha ni kwa makusudi ama tu kukosa fikra ya kutosha kujitafakari. Mara nyingi kama si zote wahusika wote tunapenda kusimulia tena kwa manung’niko ya jinsi yeye alivyo mwema, mwelewa na mzuri kwa mwenzie na kuonyesha wazi kuwa mfarakana mwenzie ni mbaya na aso faa kabisa.

Tunasahau ama tunakosa utambuzi kabisa kuwa kama kweli mwema, mwelewa na mzuri kwa mwenzio basi badala ya kulalamika, kujikosha, kutafuta kuonewa huruma na kuungwa mkono kwa hadhira ambayo hata haiihusiki kabisa; Tungeenda na kumkabili mhusika kwa kulalamika na kumwelewesha yeye ni kwa namna ipi hatakutendea haki na kuwa yapaswa muweke mambo sawa ili kufuta mfarakano huo!

Advertisements
By ashadii

Thamani inapotupwa kwa asiye thamani…

Kila mmoja ana mtu ama watu ambao ni muhimu sana katika Maisha yetu, haijalishi hao watu ni ndugu, jamaa ama marafiki. Daima hao watu  huwepo wakati wowote iwe shida ama raha… Hawa watu huwepo wakati wowote bila kujalisha hali wala mali, bila kujalisha muda wala mahala.  Ni bahati mbaya sana kuwa wengi wetu tupo wabinafsi mno kiasi kwamba huwa tuna waangalia na kuwajali wale ambao nafsi na roho zetu zinaridhia kuhangaikia – tunasahau kabisa wale ambao wapo upande wetu daima, tunasahau kuwa pale unapohitaji pa kuegemea (bila kujalisha kwa misingi ya mali ama a shoulder to lean) wale ambao hatuonyeshi kuthamini thamani yao ndio hao ambao hujitajika wakati huo; hasa wakati wa shida.

Ukiwa na bahati, ukabahatika Hekima na Busara ama tu kwa namna yoyote ukabahatika kufunguka macho na akili. Utawatambua hao watu na utawathamini pale ambapo ni muhimu wewe ukawathamini, la sivyo unaweza jikuta ukatambua thamani yao baada ya kuwapoteza baada ya kupata pengo la kukosekana kwao – Tunabaki na majuto yalojaa manung’niko kwa kutokua na namna yoyote ya kuwarudisha katika maisha yetu.

By ashadii

KUZALIWA na kuendelea KUZALIWA Upya…

Naamini kuwa mwanadamu pale tu anapozaliwa,  katika uhai wake huendelea kuzaliwa upya. Mara ngapi anazaliwa upya na ni vitu ama watu gani wanachangia kwa kuendelea kwa kuzaliwa mtu huyo kunapishana.  Kujirudia mara kwa mara kwa mwanadamu kuzaliwa upya katika maisha yake, ndivyo busara na hekima hukua ama kudidimia na kumfanya awe tofauti zaidi. Hutofauti huo kwa bahati mbaya ama nzuri unaweza kuwa kwa uzuri ama kwa ubaya tokana na maamuzi ambayo huchagua na kufanya…

Kuzaliwa upya huja pale ambapo kuna kitu ama tukio ambalo linakuwa limekugusa mno iwe kwa uzuri ama kwa ubaya kiasi kwamba hicho kitu ama hilo tukio likakubadilisha kabisa katika vitu msingi vikufafanuavyo – Iwe Msimamo /Fikra/Mtazamo/Amani ama Imani. Kuzaliwa upya huja kwa kutambua hasa kujitambua kuwa hilo suala limekubadilisha na U’mpya.

By ashadii