Tendo la ndoa na umuhimu wake kwa Wanandoa

Kuwepo na mapenzi ya dhati kati ya wanandoa hufanya mambo mengi kuwa rahisi na mepesi bila kujalisha ni kipindi cha furaha au majonzi; sababu inakuwa upo na mtu ambaye anakufanyia unafuu wa mhusika kuamini kuwa kila kitu hatimaye kitakuwa sawa mradi huyo mpenzi wako yupo karibu na wewe anakupenda na mnashirikiana vilivyo kwa kujaliana kwa misingi ya ‘Chake changu, changu chake’.

Mapenzi na kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao hasa kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu.

 Siri ya kufurahia tendo la ndoa ni wanandoa wote kuridhika na utendaji wa mwenza wao hasa wakati wa tukio, kwa kujituma, kuwa mbunifu, kutaka na kufurahia tendo hilo. Ingawa ni kweli kwa nadra inaweza tokea mwenzako akawa na hamu na wewe usiwe nayo (ikitokea mara chache sana – hili linaeleweka, na linaweza kukubalika ila si kwa kuzoea na ikawa utamaduni; iwe kwa mwanaume ama mwanamke) .

Izingatiwe kuwa, kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi rahisi… Mazingira ya kufurahia tendo hili muhimu ni lazima yajengwe na yaimarishwe mara kwa mara. Maana ni wazi kuwa uhai wa kila ambalo linatakiwa kuishi ni lazima litunzwe kwa umakini na kujali. Hivyo kufurahia tendo la ndoa pia hupaswa kuimarishwa kwa nilivyotaja hapo awali – Kupenda, kujituma, utundu, maarifa na Ubunifu. Na haya yote huwa rahisi sana ikiwa mwanandoa wako wampenda ama kumkubali, na kubwa kuliko ikiwa na yeye pia hujituma, ‘ni mtundu’ na ana maarifa pia.

 Hivi vitu (Kujituma, utundu, maarifa na ubunifu) haviji hivi hivi pia… Na ndio kwa misingi hiyo wanandoa hushauriwa kuzungumzia tendo la ndoa, kama haridhiki katika tendo, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda, wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho kinakupandisha mzuka – huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo (TAHADHARI – Yapaswa kuwa na mipaka pia).

 Mnaweza msiwe kila mmoja si mtaalam kwa mwenzie mnapoanza mahusiano yenu ya mapenzi, ila inapaswa na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ufundi huo unaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kwa mwenza wake huyo na si kupungua. Izingatiwe pia kuwa, Kufanya mapenzi si lazima ukafanya kama vile ambavyo picha za ngono huonyesha ili kujua mnafurahia, msingi ni kutafuta rhyme ambayo huwafanya wote mfurahie tendo hilo la ndoa na kuwafanya kuwa na kiu juu ya mwenza wako pale unapokuwa umemkosa.

 Ndoa si kufanya tu Mapenzi ni zaidi ya hapo, ila mwisho wa siku kufanya Mapenzi ni muhimu mno kwa ustawi wa ndoa kati ya wanandoa. Ni suala ambalo kiharaka haraka linaweza chukuliwa kwa wepesi, ila mwisho wa siku lina faida sana na FAIDA zake ni zifuatazo:

FAIDA YA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA:-

Continue reading

Advertisements

Nafasi ya MWANAMKE ndani ya ndoa…

Kwa kiasi kikubwa, tukimwangalia mwanamke wa leo na wa juzi kuna mabadiliko mengi na makubwa sana. Mabadiliko hayo yamekuwa makubwa hadi kugusa taasisi ya ndoa na nafasi yake katika ndoa hiyo.  Tamaduni na desturi zetu ziliweka misingi ya ndoa ambayo yalikuwa yanajengwa na mwanamke zaidi ya mwanaume. Ingawa ni mwanaume alitarajiwa yeye kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha mke, watoto na familia kwa ujumla inapata yaliyo msingi katika maisha ya kila siku – ni mwanamke ambaye alikuwa na nafasi ya kuhakikisha kuwa ndoa na familia ipo katika misingi thabiti na yenye nguvu kiasi kwamba kuvunjika kwa ndoa hiyo inakuwa ni mtihani.

Taasisi ya ndoa sasa hivi imebadilika sana. Bahati mbaya mwanamke amebadilika zaidi katika taasisi hiyo kuliko hata mwanaume. Mabadiliko hayo mengi ni yenye matokeo chanya kama yalivyo pia yale yenye matokeo hasi. Dhana sasa hivi imekuwa kuwa ndoa ili kufanikiwa inatakiwa jitihada ya 50/50 toka kwa wenza ili iweze simama, imarika na kudumu. Dhana hii inashikiliwa na wengi wakiwa wamesahau kuwa mafahari wawili hawezwezi kuishi zizi moja… Kwa maneno mengine usitegemee wewe kama mke ukatarajia ndoa iwe imara jitihada hizo zikiwa 50/50; mwanamke ni lazima amzidi jitihada mwanaume, ingawa pia kuna wanaume wamebarikiwa kwa jitihada ya kuweza kuimaisha ndoa zao. Ukitaka ndoa yako idumu ni lazima uwe hatua mbele kidogo kwa mume kwa yale yaliyo msingi kwa familia, na ni lazima jitihada zaki ziwe ni zaidi yake, ukubwa wa jitihada zako ndiyo bora zaidi.

Jitihada hizo huja pia na kutambua nafasi yako kama Mwanamke ndani ya ndoa ipo vipi. Majukumu yako na haki yako kama mke ni yepi na Makukumu yako na haki yako kama mama na mlezi wa familia ni yepi. Hivyo ni muhimu kutambua haya katima maeneo muhimu kwenye ndoa kuhakikisha inafanikiwa, inadumu, ina imarika na kuwa yenye furaha (ingawa huwezi kosa karaha za hapa na pale).

 BAADHI YA MAENEO MUHIMU KWA MWANAMKE KUZINGATIA KATIKA NDOA;-

Continue reading

Aina ya Wanaume WATONGOZAJI kwa vigezo vya sababu…

Kitendo cha kutongoza kina ufundi wake, na wanaume walivyo wajanja (kwa wale wenye uelewa) wana maarifa yao ya kutongoza. Maarifa hayo hutofautiana tegemeana na aina ya mwanamke ambaye wananiya ya kumtongoza. Licha ya kuwa maarifa haya yametofautiana, mwisho wa siku sababu za yeye kutongoza mwanamke huwa mle mle – sababu za msingi hufanana na moja ambayo ni kubwa kuliko zote ni tamaa.

Katika ulimwengu wa utongozaji mambo yamebadilika sasa to the extent hata akina dada/mama huwa tunajilipua once in a while. Ila ukweli unabaki bado kwa kiasi kikubwa wanao ongoza kutongoza ni akina kaka/baba. Na katika kutongoza huko wengi huwa na sababu mbali mbali za kumtongoza huyo mtongozwaji.

Zinazofuata ni sababu hizo zinazomfanya huyo kaka/baba afanye maamuzi na kufanyia kazi malengo yake ya kumpata huyo anae kuwa kadaka jicho lake. Hizi ni sababu tokana na mtazamo wangu ambazo huwa vigezo vya sababu ya kutongoza mwanamke:-

 Anakujaribu

Ni mara nyingi nimesikia kaka/baba zetu wakiweka wazi kukubaliwa na mwanamke aliye mtongoza na kukubaliwa bila kutarajia. Ni kuwa just for the sake of it, mazingira yanakuwa yanaruhusu anajikuta kutongoza kwa kujifurahisha na kujaribu alafu anajikuta mwanamke kakubali. Kama hajajipanga anatahamaki na hata kushindwa kuendeleza azma ya kukutana naye kimwili hasa kwa vinajana ambao hawana makazi badala yake hulelewa na familia hivyo kuwa na sehemu ya kukutania na mwanamke kwa ghafla ni mtihani kwake. Mwingine akikujaribu ukakubali atalala na wewe na hali mwingine atakupotezea na mwanamke akibaki akishangaa inakuwa kakubali na hatafutwi. Continue reading

By ashadii

Wapenzi wa aina hii ni HATARI kwa afya yako…

Kwa mara nyingine nashare yale niliyo nayo katika mahusiano yetu haya ya kila siku ambayo tunafurahia na wakati mwingine kutuendesha.

Ukiwa na mtu (mpenzi au rafiki, mchumba ama mwenza) mara nyingi matarajio huwa ni kufurahi na kufarijika juu ya mwenzi wako ama yale ambayo yahusiana na nyie. Mara nyingi, wengi hutaka kuwa moja ya sifa iwe mtu wake huyo awe sehemu ya maisha yake kuwa na amani na furaha kwa namna moja ama nyingine…

Kama wanadamu kukwazana hakuepukiki na wnegi wanasema ni moja ya kuimarisha mahusiano yenu. La msingi ni kuwa, hata mkikwazana vipi mna uwezo wa kurudi kwenye mstari na kuendelea na mahusiano yenu kama kawaida. Hata hivo wanadamu tumetofautiana na kuna wale ambao waweza kuwa wapenzi ila mmoja wao akawa ni mwenye tabia ya kudhoofisha afya (psychologically, physically hata emotionally) ya mwenzi wake aidha kwa makusudi ama kwa kutojitambua. Mtu wa namna hii akikuta mpenzi wake ni ‘hewalaah!’ kwa kila jambo ndipo ambapo huyo muathirika hugeuka trailer.

Kawaida hawa wapenzi ambao ni hewala maarufu kama ‘Msukule wa Mapenzi’ (in courtesy of ‘Mbu’ wa Jamiiforums) wengi sana huwa hawajitambui. Kwa maana nyingine hata wewe msomaji unaweza kuwa mmoja ya hao watu na bado ukawa hujui. Unaweza jitazama upya kwa kuangalia baadhi ya viashiria hapa chini kupima kama mwenzi wako anaimarisha ama kudhoofisha afya yako. (Zingatia kuwa mara nyingi ni kama huyo mtu ana zaidi ya traits 3/4 ama zaidi ya hizi zilizootedheshwa.)

Continue reading

By ashadii

Umewahi jiuliza upo na Mpenzi/Mwenza wako kwa sababu gani?

Upo na MPENZI/MWENZA wako kwa sababu gani?

Kuna msemo “All is fair in love and war” – ni kwa msemo huu ambao unaweza elewa maana yake – maana ingekuwa kila mmoja ana uwezo wa kusoma akili ya mtu wake kujua yupo nae kwa ajili ipi, nadhani ingekuwa balaa zaidi ya faida. Na hili ni kwako pia msomaji… Are you true to yourself? Umewahi jiuliza honestly upo na mpenzi wako kwa sababu ipi/zipi.

Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana. Wanadamu hutaka awe na wa karibu wake hasa Mpenzi kwa sababu tu kuwa anapendwa na anapenda pia. Haijalishi mpenzi huyo ni kitu gani kiliwaunganisha na kuwa wapenzi, iwe ni mapenzi ya dhati juu yake, iwe kwa ajili ya hitaji Fulani toka kwake, iwe kwa sababu ya muonekano wake – mwisho wa siku kwa wale waliopo katika mahusiano ya muda mrefu hujifunza na hatimaye kutambua kuwa mapenzi ni kiungo kimoja wapo tu cha viuongo vingi vya kuwa katika mahusiano na mtu wako huyo. Kuna viungo vingine huwepo na  pengine kuwa hata na nguvu zaidi kuliko hata kiungo cha ‘Penzi’ katika mahusiano hayo.

Mapenzi ni muhimu katika mahusiano, ila bado nafasi yake ni ndogo ukifananisha na viungo vingine. Mahusiano siku zote suala si kuangalia Mapenzi tu sababu pamoja na kuwa mapenzi ni muhimu bado yana nafasi ndogo tu katika kujenga mahusiano thabiti yaliyojaa furaha na amani. Unaweza usiwe umempenda kwa dhati mtu wako ila ukaridhika na kumkubali bila kujalisha yupo vipi ama ni wa hali gani; hilo likafanya kuwa na Amani katika mahusiano yenu alimradi na mtu wako awe hivyo pia.  Kuna watu ambao wapo pamoja na hawana mapenzi yale ya dhati na wana amani na furaha tokana na kuheshimiana, kujaliana na kuthaminiana, na hali hapo hapo kuna wale ambao wana mapenzi ya dhati na mapenzi yao yana matatizo mazito ambayo wanashindwa kabisa kuyaweka sawa kwa wao kuwa na amani katika penzi lao hilo.

Continue reading

By ashadii

Haya huwafanya baadhi ya Wanawake (Mabinti) kusita kuingia ndani ya Ndoa…

Mara ya mwisho nilizungumzia juu ya baadhi ya sababu ambazo hufanya wengi wa wanaume kusita/kusua sua kuingia katika ndoa… Leo nazungumzia upande wa pili wa shilingi… Upande wa wanawake na sababu zao za kuogopa ama kuchelewa kuingia katika ndoa.
Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.

Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)

Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.
By ashadii

Wanaume: Baadhi ya sababu ambazo huwafanya wengi waogope kuingia kwenye ndoa

Vijana wengi wa kiume hujikuta katika wakati mgumu kuchukua maamuzi ya kuishi na mwanamke japo yawezekana wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa muda mrefu kutokana na vikinza vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na vingine ni nadharia tu.

Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa. Continue reading

By ashadii Tagged

NGONO: Wanawake na Wanaume tunapoamua ‘kujiachia’ na Madhara yake…

Msomaji, nimeona vema nishirikiane nawe katika hii hoja ya kujiachia kwa miili yetu katika kufanya mapenzi na wapenzi wetu. Hapa ninaposema kujiachia sina maana kujiachia wakati wa faragha kufurahia tendo… Bali nazungumzia kujiachia kwa bahati mbaya ama makusudi na kutojali ama kuzingatia ni idadi ngapi ya watu unashirikiana nao iwe kwa siku, juma (wiki), mwezi ama hata mwaka.

Suala lililopo hapa (hasa kwa akina mama/dada) wengi hujiweka katika kundi la kutokujiachia ovyo. Kwako msomaji naomba tulia na jitafakari ukiwa mkweli kwa nafsi yako kama upo kundi hili la kujiachia.

Kujiachia kupo tofauti, kuna kujiachia unakuwa na mpenzi mmoja mmoja lakini hadumu zaidi ya miezi mitatu hivyo kukufanya uwe umelala na walau watu 4-6 kwa mwaka (hivo kama ulianza huo mchezo kaika umri wa miaka 17 na upo miaka 25 ina maana umeshawahi lala na wanaume si chini ya 25).  Pia kuna kujiachia kwa kuchanganya wapenzi ama kutoka nje ya mahusiano ya mpenzi/mwenza wako. Huku kutoka kama ni kubadilisha kila siku huko nje ndiyo kujiachia kwenyewe na nafuu huwepo kwa yule ambaye ana-maintain mtu huyo anayetoka naye. Hata hivyo tuangalie sababu ambazo hutufanya tujiachie ni zipi… Continue reading

By ashadii Tagged