Nafasi ya MWANAMKE ndani ya ndoa…

Kwa kiasi kikubwa, tukimwangalia mwanamke wa leo na wa juzi kuna mabadiliko mengi na makubwa sana. Mabadiliko hayo yamekuwa makubwa hadi kugusa taasisi ya ndoa na nafasi yake katika ndoa hiyo.  Tamaduni na desturi zetu ziliweka misingi ya ndoa ambayo yalikuwa yanajengwa na mwanamke zaidi ya mwanaume. Ingawa ni mwanaume alitarajiwa yeye kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha mke, watoto na familia kwa ujumla inapata yaliyo msingi katika maisha ya kila siku – ni mwanamke ambaye alikuwa na nafasi ya kuhakikisha kuwa ndoa na familia ipo katika misingi thabiti na yenye nguvu kiasi kwamba kuvunjika kwa ndoa hiyo inakuwa ni mtihani.

Taasisi ya ndoa sasa hivi imebadilika sana. Bahati mbaya mwanamke amebadilika zaidi katika taasisi hiyo kuliko hata mwanaume. Mabadiliko hayo mengi ni yenye matokeo chanya kama yalivyo pia yale yenye matokeo hasi. Dhana sasa hivi imekuwa kuwa ndoa ili kufanikiwa inatakiwa jitihada ya 50/50 toka kwa wenza ili iweze simama, imarika na kudumu. Dhana hii inashikiliwa na wengi wakiwa wamesahau kuwa mafahari wawili hawezwezi kuishi zizi moja… Kwa maneno mengine usitegemee wewe kama mke ukatarajia ndoa iwe imara jitihada hizo zikiwa 50/50; mwanamke ni lazima amzidi jitihada mwanaume, ingawa pia kuna wanaume wamebarikiwa kwa jitihada ya kuweza kuimaisha ndoa zao. Ukitaka ndoa yako idumu ni lazima uwe hatua mbele kidogo kwa mume kwa yale yaliyo msingi kwa familia, na ni lazima jitihada zaki ziwe ni zaidi yake, ukubwa wa jitihada zako ndiyo bora zaidi.

Jitihada hizo huja pia na kutambua nafasi yako kama Mwanamke ndani ya ndoa ipo vipi. Majukumu yako na haki yako kama mke ni yepi na Makukumu yako na haki yako kama mama na mlezi wa familia ni yepi. Hivyo ni muhimu kutambua haya katima maeneo muhimu kwenye ndoa kuhakikisha inafanikiwa, inadumu, ina imarika na kuwa yenye furaha (ingawa huwezi kosa karaha za hapa na pale).

 BAADHI YA MAENEO MUHIMU KWA MWANAMKE KUZINGATIA KATIKA NDOA;-

“MUME”

Mume ndiyo mpango mzima na ndiyo kiungo cha viuongo vyote vya ndoa yako.  Kuishi na hawa baba/kaka zetu yahitaji nguvu ya ziada. Wanadamu wanatofautiana, hivyo hata nguvu inayopaswa uitumie inatofautiana pia. Ndio maana ni muhimu na huwa ni bahati kama kweli wampenda mume wako sababu utafanya ukijua fika ndivyo utakavyo na si  tu kwa misingi kuwa imekubidi. Mumeo na haki yako kabisa, na yapaswa uitumie hiyo haki katika kumjua vizuri katika maeneo yote ya muhimu. Kujua ni wakati gani anakuwa na njaa, kujua ni kitu kipi hapendi ama anapenda, kujua mahitaji yake ya mwili na kisaikologia na muhimu zaidi ni kumsoma na kumwelewa pia. Hiyo itakusaidia kujua akiwa na njaa, akichoka, akikwazika, akiwa na msongo wa mawazo, kukiwa na kitu kinamsumbua, akiwa na dalili ya kuumwa, akiwa na furaha na mengine mengi. Ukiweza kufaulu hapo unakuwa umefaulu mengi kwa upana na kukufanyia wepesi katika majukumu yako ndani ya nyumba kama mke.

 “NYUMBANI”

Haijalishi uwezo wenu wa kifedha na hali yenu kimaisha, nyumbani kwako ni sehemu muhimu sana kuweka mazingira ambayo ni masafi, mazuri, na tulivu. Unaweza usiwe na vitu vingi wala usiwe na vitu vya thamani ila mpangilio mzuri na usafi pakafanya nyumbani hapo pawe mahala pa amani na pakuweza kupumzikia bila kikwazo chochote. Hili linaweza kwa namna moja ama nyingine pia kuchangia kwa mume kutambua kuwa pale anapo taka utulivu na amani nyumbani ni mahala bora zaidi kuliko akifikiria mahala pengine.

“MATUMIZI YA NDANI/NYUMBANI”

Matumizi mazuri ni sehemu ya muhimu katika ndoa. Wanandoa wengi baadhi ya vyanzo vikubwa vya ugomvi ni kutokuwepo pesa ya kutosha ama utumiaji mbaya wa pesa hiyo. Hili linaweza kuwa kwa mke na mume pia. Hata hivyo ni muhimu kwa mwanamke kutambua kuwa akiwa na kiu ya maendeleo na mafanikio kwa familia yake basi atakuwa mtumiaji mzuri wa pesa na mshauri mzuri kwa mume katika kupanga matumizi ya pesa. Bila kujalisha kama pesa hiyo inatafutwa na wote ama mmoja wa wenza hao. Wanawake wengi tuna madhaifu ya kununua kitu hata kama uhitaji sababu tu labda bei ni nafuu, au ulikuwa na shoga nae alinunua, au tu muuziaji alifaulu kukushawishi kununua. Ni vema mwanamke ukajua bajeti yako ya matumizi ya familia kwa week/mwezi ni kiasi kipi, na  ni vizuri kujenga desturi ya kuorodhesha mahitaji yako ya kununua unapokuwa unaenda kufanya manunuzi makubwa iwe ya ndani ama tu mahitaji binafsi. Hili linaepusha kutumia pesa nyingi kuliko na hata pia kununua kitu uisicho dhamiria kuwa nacho kwa wakati huo.

 “NDUGU NA JAMAA”

Kuna msemo kuwa mradi mume na mke wapendana, hilo tu ndiyo muhimu hivyo wengine hayawahusu. (Hili kundi la hayawahusu mara nyingi huwa ni dongo kwa wanandungu) suala ambalo si zuri na ni hatari kwa hapo baadae. Ni muhimu kama mke ukatambua kuwa ndugu wa mume wana umuhimu na maana kubwa kwa mumeo hivyo yapaswa kuwa na kwako pia. Na ni vizuri kutambua huyo mume umemjua ukubwani na hali hao ndugu zake wametoka mbali si haki kabisa kuwagombanisha na kuwakosanisha.

Kuishi vizuri na ndugu na jamaa (hivo uvumilivu wa madhaifu yao hata yakivuka mpaka ni muhimu) Mtu ambae huishi nae anakuboa kila mara, ni rahisi kumvumilia. Na hata hivo zingatia kua sio ndugu woote wa Mwenza wako wana hila, saa ingine Mke ndo huanzisha na kusababisha hizo hila… Wakija wageni wake unavimba… Unataka wa upande wako tu, Usithubutu dear…. Kuna ile pia ya ngugu wa mumeo (kama vile dadake na Mamake) kutaka shindana kuchukua attention ya mumeo; ukilogwa ukaingia katika mashindano hayo ni muhimu utambue kuwa atakae umia katika ugomvi huo zaidi kuliko wote ni mpenzi wako ambaye ndiyo mume wako. Saa ingine ni vema kujifanya mjinga kama haikupunguzii kitu ili kumlinda mumeo.

“UPENDO/MAPENZI NDANI YA NDOA”

Mapenzi ndani ya ndoa hayapo hayafanani siku zote, hua yanabadilika na kwa wengine kunatokea wakati hadi mmoja wenu akahisi anamchukia kabisa mwenza wake. Ndani ya mahusiano ya mapenzi, kuna wakati mapenzi hupungua, hufa, na kuweza kuongezeka mara dufu. Kubadilika huko mara nyingi huwa ni mapito tu na yapaswa kuongeza jitihada na kujituma kutoa giza hilo. Matatizo kama haya kama kwa matatizo mengine yasikujenge kichwani kudhania ndoa ndiyo imekufa na kutaka kuachia ngazi na kusonga mbele. Yapaswa kuwa mstahimilivu, kua mvumilivu, kua mwerevu na jitahidi saana kua mke mwenye busara na asokurupuka…. Na hiyo yawezekana tu kwa kumhusisha Mungu katika ndoa yako…. HOWEVER Inapotokea uvumilivu wako hauzai matunda na hali kuzidi kuwa mbaya kiasi kwamba unaona kabisa hakuna namna ya kuweza kuweka mambo sawa, ni vizuri kukubali ukweli kuwa imeshindikana na yapaswa uangalie mbinu ama maamuzi mengine ya kuchukua.

“UGOMVI NDANI YA NYUMBA”

Usije jisahau ukajiona you are so special na kwamba wee tu ndo mwangombana na mumeo (incase ikatokea); Usipende saana kuhusisha mambo ya ugomvi wako na watu wengine – unless otherwise issue ni kubwa saana. BUT hata hivo inabidi unakua makini ni nani umhusishe… Yahitaji sana mtu mwenye busara, hekima na nia njema juu yako kuweza kusaidia kweli matatizo yaliyopo ndani ya ndoa yako. Na ule mtindo wa kusimulia saa ingine wajichora na kumfanya mtu ambae unamsimulia afurahi katika roho yako – na pia wewe mwenyewe unakua unajenga upenyo wa kuletewa mambo ambayo yaweza athiri ndoa yako.

“MARAFIKI/MASHOGA”

Marafiki ni wa kuwa makini nao sana. Sisemi kuwa usiwe na rafiki ila huyo rafiki ni muhimu kukawa na mipaka katika urafiki wengu hasa katika masuala yanayohusiana na ndoa yako. Marafiki dear hasa mashoga tena shoga zako ambao hawajawahi olewa ndo sumu kabisa.

Mnakuwa na majukumu tofauti, katika yale ya msingi mara nyingi mitazamo tofauti na mara nyingi mtu wa namna hii hata kumhusisha kutaka ushauri unao husu mahusiano ya ndoa yako si mzuri sana kumtumia.  Inapaswa kuwa makini sana. Shoga anakua shogaa mpaka mwazoeana aje nyumbani hadi chumbani kwako na mumeo…. Aingie apike jikoni hicho chakula aandaliwe na mumeo (na hali huna lolote la kukuzuia wewe mwenyewe kufanya)….. Shoga ajue siri zako zoote za wewe na mumeo hadi zile intimate as in what makes him tick…. Shoga wa kuja kila week nyumbani kwako…. Shoga wa kumuachia wana hug, tia story (bila uwepo wako) na mumeo, peana lift za ovyo ovyo (in the name ya usasa or whatever) HAKUFAI Period!! Hawa in most cases ndo hugeuka the next wife to your hubby, na ndo wasaliti wakubwa ambao hata akimkamata mumeo aweza shindwa furukuta for tayari ajua the inns na outs zoote za huyo mwanaume…..

“TENDO LA NDOA”

Tendo la ndoa ni moja ya kuingo muhimu katika ndoa. Ni moja ya kitu ambacho mtajaaliwa kukifurahia kila pale mtakapo, katika eneo hili kama mke yapaswa kujituma, kuwa mbunifu, kupenda na kulipenda tendo lenyewe ili kulifurahia. Ni muhimu ukalipa nafasi na usiwe moja ya wanawake ambao tendo la ndoa kufanya kwao kama adhabu. Ni muhimu mkajenga utamaduni wa kuwa huru na kujiachia kwa mumeo na yeye kwako ili kuweza kusomana, nini kila mmoja anapenda, nini kila mmoja hapendi, ni wapi kila mmoja anapenda aguswe, ni vipi kila mmoja anapenda akunwe. Yapaswa siku zinavyo zidi kwenda ndivyo hata kufurahia na kujuana miili yenut inavyokuwa, na hakuna haja ya kutaka kufanya mapenzi ya kuiga (kwa wale wanaodhani kuwa Porn ndiyo jawabu – Labda kama ni Kamasutra ambao wamefanya kwa ustaarabu). Tafuteni rhyme yenu ya kuweza kujilia ni namna ipi mwafurahia zaidi.

“CHAKULA”

Chakula kwa mume na famila ni kitu cha msingi sana.  Kumekuwa na idadi kubwa ya wanaume katiak jamii wakilalamika mapishi ya wake zao na hata kuona bora kule nje badala ya nyumbani hata kama ana uwezo wa kununua kila kitu.  Wanaume wengi wanapenda Sex, Chakula kizuri na vinywaji, mengine hufuata. Ninapo sema vinywaji sina maana tu pombe, mume anapo shinda nyumbani siku hiyo ni muhimu kati ya mida ya chakula kunakuwa na vinywaji kama Chai, Kawaha na hata Juice.

Chakula pia kinaweza haribu mahusiano hasa kati ya wenza/wapenzi… Hii hutokea saana pale mdada/mmama mapishi nyumbani kwake yamemshinda kabisaa… In short hajui kupika… wakaka/baba wengine hawana makuu na huvumilia na kuona sawa tu… (ni wachache by the way…) BUT Issue ni kwa wale ambao kalelewa katika familia ambayo they are Great Cooks… yaani kazoea chakula kizuri na kitamu pia… yaani hata kama kala tu Ugali na dagaa… huo ugali ni ugali umesongwa hasa!… na hizo dagaa mazagazaga yoote from kitunguu saumu, nazi, nyanya/hoho/carrot/vitunguu, curry powder to perfection. (Huyu akipata nyumba ndogo anajua wajibu wake katika sector ya chakula usishangae ukitangaziwa mke mdogo….)salads. Of course bila kusahau Matunda na Home made fresh Juice – for vitu kama soda, wine, beer not recommended kuenda sambamba na food…

“WEWE MWENYEWE MWANAMKE/TABIA”

Jitambue, Jipende, Jithamini na Furahia maisha!  Huwezi kufurahia misha hata ukiwa na mume akupendae na akakupa kila kitu ikiwa hujajitambua, hujajipenda na hujithamini. Ukiwa na hayo… Ina maana utatambua nafasi yako kama mke na mama, utajua nini unataka na  ni namna ipi ukipate.

Haya yatakusaidia katika tabia pia. Hutakuwa moja ya wale wanawake wa kununa kila saa kwa mume bila sababu za msingi, mwanamke mlalamishi kwa kila kitu, mwanamke gubu kila siku ya Mungu na tabia nyingi ambazo zinaweza kufanya hata mwenza wako akuchoke haraka na kukuona ni kero badala ya faraja katika maisha yake.

Siyo rahisi kuji tathimini, ila ni muhimu kujaribu.

Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s