‘HUSUDA’ inapogeuka Chuki…

Husuda hukua, hushamiri na hata ufa kabisa. Mara nyingi husuda juu ya mhusudiwa hujengwa na kukua tokana na namna mhusudiwa alivyo hasa ikiambatana na sifa zake zimvutiazo mhusudu. Kila mmoja huwa na mtu anae mhusudu iwe kwa uwazi au kwa siri… Inapotokea husuda hiyo ikakithiri hujigawa njia mbili ambayo kila mhusudu lazima ashike mojawapo ya hizo njia.

Njia ya kwanza – huwa Mapenzi nyoofu na ya dhati ya mhusudu kwa mhusudiwa. Mapenzi hayo hujengwa na Imani ndani ya nafsi ya mhusudu kua mhusudiwa anastahili na ana haki ya kujaaliwa kuwa na Sifa hizo silizomfanya mhusudu kumpenda mhusudiwa. Hutamani kwa nia njema awe kama mhusudiwa huku akimuombea azidi kibarikiwa.

Njia ya pili – huwa chuki ya kawaida ama iliyokithiri ya Mhusudu kwa Mhusudiwa. Chuki hiyo hujengwa na imani ndani ya nafsi ya Mhusudu kua Mhusudiwa hastahili, hana la ziada ama sababu za msingi kujaaliwa kuwa na Sifa hizo zilizomfanya amchukie kwa kutaka Sifa za Mhusudiwa ziwe zake yeye huku akimuombea mabaya pengine hat a kumwendea kwa mganga amwangamize… Hili kufanya ‘husuda’ ya Mhusudu kuwa CHUKI kwa Mhusudiwa.

Tuwe makini na husuda zetu.

Advertisements

2 comments on “‘HUSUDA’ inapogeuka Chuki…

 1. Mada hii inanikumbusha dhana ya ‘Hate Love relationship’. Yaani Mtu anahusudu kwa dhati kabisa na kwa moyo wote. Tatizo linakuja kwa yule anayehusudiwa. Mhusudu anaweza kuja kugindua kuwa alivyodhani sivyo. Mhusudiwa anaweza kuwa na mapumgufu makubwa sana anaweza kuwa ni mtu asiyeweza kukaa na mpenzi mmoja, anaweza kuwa mlevi na tabia nyingine ambazo mhusudu alikuwa hajazitambua.

  Kwa kugundua hivyo Mhusudu atajikuta kwenye CHUKI dhidi ya mhusudiwa. Lakini inashangaza kwa nini pamoja na CHUKI hizo bado Mhusudu anashindwa kabisa kuachana na Mhusudiwa.

  Kwa wakati mmoja ANAHUSUDU na KUCHUKIA kwa pamoja. Mifano halisi huwa ipo, mhusudu analalama na kuomboleza juu ya mapungufu ya Mhusudiwa lakini kwa namna ya mshangao sana wanazidi kuwa pamoja.

  Wataalamu wanasema kuna wakati CHUKI inakuwa kama Sumaku ya kuunganisha haiba. Yaani kinachowaunganisha hawa sio HUSDA ila ni CHUKI. Suluhu ya kutengana au ukitaka kuachana na Mpenzi wa namna hiiyo lazima UONDOE CHIKI KWANZA DHIDI YAKE … ndipo utaweza Kumucha au kumsaidia. lol!

  • AJ, Nimependa saana maelezo yako. Hasa inavyoshangaza pale Mhusudu anaposhindwa kujiweka mbali na Mhusudiwa pale inapotokea anamchukia kabisa.

   Hii kimsingi si nzuri kwa Mhusudu na Mhusudiwa pia. Kuna wengine roho zao kujenga chuki zaidi na zaidi inaweza kuza wazo la kuharibu na kuangamiza kabisa kwa Mhusudiwa. Unashangaa watu ambao walikua karibu na hata pengine marafiki kumgeuka na kumsaliti kwa matendo mabaya kabisa Mhusudiwa.

   Nadhani hili ndilo hata chimbuko la mseom “Kikulacho ki nguoni mwako”. Unaweza kutwa na maswaibu ambayo yamepandikizwa na mtu wako wa karibu, mhusika akajua or asijue kabisa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s