Image

Nelson Mandela – Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Nelson Mandela - Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Mtu akiwa hai ama akifariki, hasa kama kakugusa ndani ya moyo na nafsi yako bila kujalisha ni ndugu ama si ndugu, wanadamu wengi tuna kasumba ya kutaka kumwombea kheri na kila kizuri kimfikie kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo kuna watu wachache walibarikiwa na wamebarikiwa kiasi kwamba ukitata kumuombea kwa kutaja ni vipi abarikiwe, aneemeshwe ama kujaaliwa unashindwa kabisa kujua ni lipi wewe mwanadamu mwenzie unaweza kumuombea…

Badala ya kumwombea yeye, unabaki ukiishia kujiombea mwenyewe kwa madhaifu mengi uliyo nayo, mapungufu mengi uliyo nayo, umri mdogo ulio nao, kwa kutamani na kuomba kwa dhati kwa Mwenyezi Mungu akubariki kama alivyo mbariki huyo ambae haswa ulitaka kumwombea.

Nelson Mandela ni mmoja wa hao watu, waliobarikiwa busara na hekima za hali ya juu; kua na uwezo wa kugusa nyoyo za wengi, wanaomjua kwa karibu na wasiomjua, aliefanikiwa kukusanya heshima za mataifa mbali mbali, aliefanikiwa kuonyesha thamani ya maisha iwapo mwanadamu ataishi kwa kutaka na kusimamia yaliyo bora kwa wote na si kwake tu.

Kafanya mengi na kuishi maisha marefu kiasi kwamba kifo chake sasa akiwa na umri wa miaka 95 yapaswa kuwa wakati wa kufurahi na kumshukuru Mungu kwa uwepo wake hapa duniani na kwa yale aliyofanya. Kifo chake twapasa kushukuru na kutambua alichoka na alihitaji pumziko la milele na Amani kwa kazi ngumu, nzuri na ya yamanufaa aliyofanya. Jina lake daima litadumu mioyoni mwa wengi.

Pumzika kwa Amani Madiba, for you have lived life to the fullest.

Advertisements
By ashadii