Image

Nelson Mandela – Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Nelson Mandela - Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Mtu akiwa hai ama akifariki, hasa kama kakugusa ndani ya moyo na nafsi yako bila kujalisha ni ndugu ama si ndugu, wanadamu wengi tuna kasumba ya kutaka kumwombea kheri na kila kizuri kimfikie kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo kuna watu wachache walibarikiwa na wamebarikiwa kiasi kwamba ukitata kumuombea kwa kutaja ni vipi abarikiwe, aneemeshwe ama kujaaliwa unashindwa kabisa kujua ni lipi wewe mwanadamu mwenzie unaweza kumuombea…

Badala ya kumwombea yeye, unabaki ukiishia kujiombea mwenyewe kwa madhaifu mengi uliyo nayo, mapungufu mengi uliyo nayo, umri mdogo ulio nao, kwa kutamani na kuomba kwa dhati kwa Mwenyezi Mungu akubariki kama alivyo mbariki huyo ambae haswa ulitaka kumwombea.

Nelson Mandela ni mmoja wa hao watu, waliobarikiwa busara na hekima za hali ya juu; kua na uwezo wa kugusa nyoyo za wengi, wanaomjua kwa karibu na wasiomjua, aliefanikiwa kukusanya heshima za mataifa mbali mbali, aliefanikiwa kuonyesha thamani ya maisha iwapo mwanadamu ataishi kwa kutaka na kusimamia yaliyo bora kwa wote na si kwake tu.

Kafanya mengi na kuishi maisha marefu kiasi kwamba kifo chake sasa akiwa na umri wa miaka 95 yapaswa kuwa wakati wa kufurahi na kumshukuru Mungu kwa uwepo wake hapa duniani na kwa yale aliyofanya. Kifo chake twapasa kushukuru na kutambua alichoka na alihitaji pumziko la milele na Amani kwa kazi ngumu, nzuri na ya yamanufaa aliyofanya. Jina lake daima litadumu mioyoni mwa wengi.

Pumzika kwa Amani Madiba, for you have lived life to the fullest.

Advertisements
By ashadii

One comment on “Nelson Mandela – Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

  1. AshaDii,

    ‘Ukombozi Wa Roho’ Ni Msemo alioutumia Rais Kikwete katika moja ya Sifa akizokuwa ananuelezea Hayati Mandela siku ya kusherehekea miaka 52 ya Uhuru Wa Tanzania.

    Nilifurahi jinsi Rais Kikwete alivyoifafanua dhana hiyo. Kwani kwangu pamoja na sifa nyingi mno alizokuwa nazo Mandela hiyo ya uwezo wa kuwezesha ukombozi wa Roho kupitia Truth and Reconciliation sintamsahau Mandela.

    Naamini alikuwa na UKOMBOZI WA ROHO .. ambao ni Utu wa mwanadamu, ndio maana aliweza kuusababisha kwa binaadamu wengine.

    Watanzania tumuenzi kwa vitendo kwa kudumisha dhana ya Utu wa Taifa letu ambao ni matunda ya Ukombozi wa Roho Kama alivyosimulia Rais Kikwete.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s