Kuhamasisha mabadiliko kwa Mwanamke katika maisha ya kila siku….

Image

Leo, Machi 8, 2014 ni Siku ya Wanawake Duniani. Ujumbe kwa wanawake wote mwaka huu ni “Inspiring Change”.

Mabadiliko katika maisha huwa mazuri ama mabaya (negative or positive results). Mabadiliko huja kwa namna mbili katika maisha ya mwanadamu yeyote yule:

Mabadiliko ya aina ya kwanza huja yenyewe tokana na mazingira yaliyokuzunguka, watu waliokuzunguka na namna na mahala unapoishi. Mabadiliko ya namna hii huweza kuwa mabadiliko mazuri au mabadiliko mabaya. Bila kujalisha uzuri au ubaya wa mabadiliko hayo mara nyingi hubadilisha kabisa maisha kwa raha ama karaha.

Mabadiliko ya aina ya pili huja kwa kunuia na kukusudia. Uzuri wa mabadiliko haya ya kukusudia daima hulenga mafanikio, hakuna ambaye husududia katika maisha yake afanya mabadiliko ya kujidhoofisha mafanikio  yake. Mabadiliko haya huambatana na mipango madhubuti ikilenga kuweka wepesi katika maisha kwa namna yoyote ile. Kuanikiwa ama kutofanikiwa kwa mipango hiyo ni masuala mengine lakini mwisho wa siku jitihada inayowekwa katika kuhakikisha malengo yanatimia ndio msingi wa mafanikio yenyewe.

Mwanamke kwa kiasi kikubwa na jamii nyingi amekuwa ni mtu wa kukandamizwa, suala ambalo limeenda likipungua kwa kiasi kikubwa sana lakini kwa taratibu miaka inavyozidi kusonga mbele. Katika jamii nyingi ambazo mwanamke amekuwa akikandamizwa; masuala mengi ukifuatilia kwa karibu – kiini cha makandamizo hayo ni mwanamke mwenyewe licha ya kuwa jamii nayo inabeba lawama katika kufanikisha hilo.

Hali hii (kukandamizwa kwa mwanamke) inaweza kutokomezwa endapo mwanamke mwenyewe akiamua anataka mabadiliko hayo. Mabadiliko hayo hayataweza kuja bila mwanamke mwenyewe kujitambua thamani yake; hayataweza kufanikiwa endapo mwanamke mwenyewe hatajua umuhimu wake katika jamii yake na kamwe hayawezi kufanikiwa endapo mwanamke huyo hatakuwa na nia ya kupata mabadiliko hayo.

Wanawake wenzangu nawasihi tudhamirie kufanya mabadiliko yenye kutuwekea wepesi na kufanya unafuu katika maisha yetu na wenzetu wote. Mabadiliko hayo kuweza kufanikiwa kutakuja kwa wanawake wote kutambua inapaswa tuboreshe nafasi, heshima na wajibu wetu katika jamii.

Kwa wale ambao tayari wamefanikiwa kujikwamua, bado wana kazi kubwa ya kuwakwamua wengi ambao wanahitaji msaada na kushikwa mkono ili kuweza kuleta mabadiliko. Nawatakia wanawake wote kufanikisha azma yao ya kuweza kuleta mabadiliko kuanzia siku hii ya Wanawake Duniani.

Advertisements
By ashadii

2 comments on “Kuhamasisha mabadiliko kwa Mwanamke katika maisha ya kila siku….

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s