Kuhamasisha mabadiliko kwa Mwanamke katika maisha ya kila siku….

Image

Leo, Machi 8, 2014 ni Siku ya Wanawake Duniani. Ujumbe kwa wanawake wote mwaka huu ni “Inspiring Change”.

Mabadiliko katika maisha huwa mazuri ama mabaya (negative or positive results). Mabadiliko huja kwa namna mbili katika maisha ya mwanadamu yeyote yule:

Mabadiliko ya aina ya kwanza huja yenyewe tokana na mazingira yaliyokuzunguka, watu waliokuzunguka na namna na mahala unapoishi. Mabadiliko ya namna hii huweza kuwa mabadiliko mazuri au mabadiliko mabaya. Bila kujalisha uzuri au ubaya wa mabadiliko hayo mara nyingi hubadilisha kabisa maisha kwa raha ama karaha.
Continue reading

By ashadii

Kuna Mapenzi ya kweli kati yako na Mpenzi wako? (Do you feel Loved?)

Upo kwenye mahusiano ya Kimapenzi? Unahisi unapendwa na mpenzi wako? Haya ni mwaswali ya kujiuliza kuelewa hii Makala.

Katika mahusiano wengi kama si wote hupenda kuelewa mpenzi wake anampenda kiasi kipi, pengine saa ingine hata kutamani angekuwa na uwezo wa kuona nafsi ya mpenzi wake huyo ni kwa kiasi kipi penzi hilo limetawala; bahati mbaya ama nzuri haiwezekani.  Hata hivyo kuna dalili katika mahusiano kati ya wawili ambazo uashiria endapo mpenzi wako huyo anakupenda ama lah. Hii huambatana na kutokana na tabia na nyenendo za mpenzi wako huyo dhidi yako.

Do u feel loved

Baadhi ya viashiria ambavyo vinaweza kukusaidia katika kutafakari ama kutambua endapo Mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda.

Mawasiliano egemezi kati yenu (Communication)

Hii ni mawasiliano kwa njia za viwezesha mawasiliano hasa simu. Sasa hivi mawasiliano yamerahisishwa mno ikiwa na njia nyingi kama vile kupiga simu, njia za messages hasa kama vile Whatsapp, Viber, Skype na text messages. Kwa yeyote aliye na simu ya mkononi ni rahisi kuwasiliana na mpenziwe wakati wowote ule. Mawasiliano ni njia moja wapo ya muhimu sana katika kujenga na kuboresha mawasiliano kati ya wapenzi. Inapotokea mawasiliano hayo yame elemea Zaidi upande mmoja siku zote; hapo kidogo ni tatizo. Kimsingi mawasiliano hupaswa kuwiana (mtu na mpenzi wake wote watafutane kwa usawa) ingawa inaweza pishana kidogo tokana na sababu mbali mbali. Ila inapotokea siku zote mpenzi wako huyo katka mawasiliano hufanya haya;

–          Hakutafuti siku zote hadi uanze wewe.

–          Kukukatia simu na kukuzimia bila maelezo yoyote ya msingi.

–          Kuwa mkali kila ukimtafuta, kukuonyesha kana kwamba simu zako kwake ni kero.

–          Kuchukua mda mrefu kujibu jumbe zako ama kutojibu kabisa na hata ukimuuliza hakuna sababu za msingi.

*Kwa baadhi ya tabia hizo katika mawasiliano ni dalili ambazo zinachangia kuonyesha kuwa mpenzi wako huyo hakupendi. Na hasa ikiwa tabia hizo zote anazo zote.

Continue reading

Image

Nelson Mandela – Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Nelson Mandela - Wachache ya Waliobarikiwa kwa kila kitu

Mtu akiwa hai ama akifariki, hasa kama kakugusa ndani ya moyo na nafsi yako bila kujalisha ni ndugu ama si ndugu, wanadamu wengi tuna kasumba ya kutaka kumwombea kheri na kila kizuri kimfikie kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo kuna watu wachache walibarikiwa na wamebarikiwa kiasi kwamba ukitata kumuombea kwa kutaja ni vipi abarikiwe, aneemeshwe ama kujaaliwa unashindwa kabisa kujua ni lipi wewe mwanadamu mwenzie unaweza kumuombea…

Badala ya kumwombea yeye, unabaki ukiishia kujiombea mwenyewe kwa madhaifu mengi uliyo nayo, mapungufu mengi uliyo nayo, umri mdogo ulio nao, kwa kutamani na kuomba kwa dhati kwa Mwenyezi Mungu akubariki kama alivyo mbariki huyo ambae haswa ulitaka kumwombea.

Nelson Mandela ni mmoja wa hao watu, waliobarikiwa busara na hekima za hali ya juu; kua na uwezo wa kugusa nyoyo za wengi, wanaomjua kwa karibu na wasiomjua, aliefanikiwa kukusanya heshima za mataifa mbali mbali, aliefanikiwa kuonyesha thamani ya maisha iwapo mwanadamu ataishi kwa kutaka na kusimamia yaliyo bora kwa wote na si kwake tu.

Kafanya mengi na kuishi maisha marefu kiasi kwamba kifo chake sasa akiwa na umri wa miaka 95 yapaswa kuwa wakati wa kufurahi na kumshukuru Mungu kwa uwepo wake hapa duniani na kwa yale aliyofanya. Kifo chake twapasa kushukuru na kutambua alichoka na alihitaji pumziko la milele na Amani kwa kazi ngumu, nzuri na ya yamanufaa aliyofanya. Jina lake daima litadumu mioyoni mwa wengi.

Pumzika kwa Amani Madiba, for you have lived life to the fullest.

By ashadii

‘HUSUDA’ inapogeuka Chuki…

Husuda hukua, hushamiri na hata ufa kabisa. Mara nyingi husuda juu ya mhusudiwa hujengwa na kukua tokana na namna mhusudiwa alivyo hasa ikiambatana na sifa zake zimvutiazo mhusudu. Kila mmoja huwa na mtu anae mhusudu iwe kwa uwazi au kwa siri… Inapotokea husuda hiyo ikakithiri hujigawa njia mbili ambayo kila mhusudu lazima ashike mojawapo ya hizo njia.

Njia ya kwanza – huwa Mapenzi nyoofu na ya dhati ya mhusudu kwa mhusudiwa. Mapenzi hayo hujengwa na Imani ndani ya nafsi ya mhusudu kua mhusudiwa anastahili na ana haki ya kujaaliwa kuwa na Sifa hizo silizomfanya mhusudu kumpenda mhusudiwa. Hutamani kwa nia njema awe kama mhusudiwa huku akimuombea azidi kibarikiwa.

Continue reading

Fahamu namna ya kutambua na kuboresha penzi la kweli

 

Chris Mauki ni mtaalam wa saikolojia na Mwalimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliyebobea katika tasnia ya saikolojia ya mahusiano, ndoa, malezi, kazi na mawasiliano.

Kwa miaka mingi sasa Chris amekuwa akitumia muda wengi kuzungumza na makundi mbalimbali ya watu ndani na nje ya Tanzania kwa lengo la kuboresha mahusiano, kurudisha amani iliyotoweka ndani ya mioyo ya watu na kuwawezesha watu mbalimbali kufikia malengo yao ikiwa ni pamoja na viongozi, walio makazini na katika biashara kwa kuboresha namna wanavyofikiri na namna wanavyojenga mahusiano na watu wengine.

Chriss ni mmoja wa wazungumzaji na waandishi katika Jopo la Wataalam wa Afrika Mashariki (East Africa Speakers Bureau) na katika DVD hii iliyoandaliwa na 24 Hrs Media, Chris anazu

ngumzia namna ya kutambua na kuboresha penzi la kweli. DVD hii ya saa moja itakuwa madukani hivi karibuni na kwa maelezo zaidi wasiliana na East Africa Speakers Bureau (EASB) kupitia info@eastafricaspeakers.net au piga simu +255 22 2700051/717 653544.

By ashadii

Tendo la ndoa na umuhimu wake kwa Wanandoa

Kuwepo na mapenzi ya dhati kati ya wanandoa hufanya mambo mengi kuwa rahisi na mepesi bila kujalisha ni kipindi cha furaha au majonzi; sababu inakuwa upo na mtu ambaye anakufanyia unafuu wa mhusika kuamini kuwa kila kitu hatimaye kitakuwa sawa mradi huyo mpenzi wako yupo karibu na wewe anakupenda na mnashirikiana vilivyo kwa kujaliana kwa misingi ya ‘Chake changu, changu chake’.

Mapenzi na kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao hasa kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu.

 Siri ya kufurahia tendo la ndoa ni wanandoa wote kuridhika na utendaji wa mwenza wao hasa wakati wa tukio, kwa kujituma, kuwa mbunifu, kutaka na kufurahia tendo hilo. Ingawa ni kweli kwa nadra inaweza tokea mwenzako akawa na hamu na wewe usiwe nayo (ikitokea mara chache sana – hili linaeleweka, na linaweza kukubalika ila si kwa kuzoea na ikawa utamaduni; iwe kwa mwanaume ama mwanamke) .

Izingatiwe kuwa, kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi rahisi… Mazingira ya kufurahia tendo hili muhimu ni lazima yajengwe na yaimarishwe mara kwa mara. Maana ni wazi kuwa uhai wa kila ambalo linatakiwa kuishi ni lazima litunzwe kwa umakini na kujali. Hivyo kufurahia tendo la ndoa pia hupaswa kuimarishwa kwa nilivyotaja hapo awali – Kupenda, kujituma, utundu, maarifa na Ubunifu. Na haya yote huwa rahisi sana ikiwa mwanandoa wako wampenda ama kumkubali, na kubwa kuliko ikiwa na yeye pia hujituma, ‘ni mtundu’ na ana maarifa pia.

 Hivi vitu (Kujituma, utundu, maarifa na ubunifu) haviji hivi hivi pia… Na ndio kwa misingi hiyo wanandoa hushauriwa kuzungumzia tendo la ndoa, kama haridhiki katika tendo, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda, wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho kinakupandisha mzuka – huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo (TAHADHARI – Yapaswa kuwa na mipaka pia).

 Mnaweza msiwe kila mmoja si mtaalam kwa mwenzie mnapoanza mahusiano yenu ya mapenzi, ila inapaswa na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ufundi huo unaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kwa mwenza wake huyo na si kupungua. Izingatiwe pia kuwa, Kufanya mapenzi si lazima ukafanya kama vile ambavyo picha za ngono huonyesha ili kujua mnafurahia, msingi ni kutafuta rhyme ambayo huwafanya wote mfurahie tendo hilo la ndoa na kuwafanya kuwa na kiu juu ya mwenza wako pale unapokuwa umemkosa.

 Ndoa si kufanya tu Mapenzi ni zaidi ya hapo, ila mwisho wa siku kufanya Mapenzi ni muhimu mno kwa ustawi wa ndoa kati ya wanandoa. Ni suala ambalo kiharaka haraka linaweza chukuliwa kwa wepesi, ila mwisho wa siku lina faida sana na FAIDA zake ni zifuatazo:

FAIDA YA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA:-

Continue reading

Nafasi ya MWANAMKE ndani ya ndoa…

Kwa kiasi kikubwa, tukimwangalia mwanamke wa leo na wa juzi kuna mabadiliko mengi na makubwa sana. Mabadiliko hayo yamekuwa makubwa hadi kugusa taasisi ya ndoa na nafasi yake katika ndoa hiyo.  Tamaduni na desturi zetu ziliweka misingi ya ndoa ambayo yalikuwa yanajengwa na mwanamke zaidi ya mwanaume. Ingawa ni mwanaume alitarajiwa yeye kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha mke, watoto na familia kwa ujumla inapata yaliyo msingi katika maisha ya kila siku – ni mwanamke ambaye alikuwa na nafasi ya kuhakikisha kuwa ndoa na familia ipo katika misingi thabiti na yenye nguvu kiasi kwamba kuvunjika kwa ndoa hiyo inakuwa ni mtihani.

Taasisi ya ndoa sasa hivi imebadilika sana. Bahati mbaya mwanamke amebadilika zaidi katika taasisi hiyo kuliko hata mwanaume. Mabadiliko hayo mengi ni yenye matokeo chanya kama yalivyo pia yale yenye matokeo hasi. Dhana sasa hivi imekuwa kuwa ndoa ili kufanikiwa inatakiwa jitihada ya 50/50 toka kwa wenza ili iweze simama, imarika na kudumu. Dhana hii inashikiliwa na wengi wakiwa wamesahau kuwa mafahari wawili hawezwezi kuishi zizi moja… Kwa maneno mengine usitegemee wewe kama mke ukatarajia ndoa iwe imara jitihada hizo zikiwa 50/50; mwanamke ni lazima amzidi jitihada mwanaume, ingawa pia kuna wanaume wamebarikiwa kwa jitihada ya kuweza kuimaisha ndoa zao. Ukitaka ndoa yako idumu ni lazima uwe hatua mbele kidogo kwa mume kwa yale yaliyo msingi kwa familia, na ni lazima jitihada zaki ziwe ni zaidi yake, ukubwa wa jitihada zako ndiyo bora zaidi.

Jitihada hizo huja pia na kutambua nafasi yako kama Mwanamke ndani ya ndoa ipo vipi. Majukumu yako na haki yako kama mke ni yepi na Makukumu yako na haki yako kama mama na mlezi wa familia ni yepi. Hivyo ni muhimu kutambua haya katima maeneo muhimu kwenye ndoa kuhakikisha inafanikiwa, inadumu, ina imarika na kuwa yenye furaha (ingawa huwezi kosa karaha za hapa na pale).

 BAADHI YA MAENEO MUHIMU KWA MWANAMKE KUZINGATIA KATIKA NDOA;-

Continue reading

Aina ya Wanaume WATONGOZAJI kwa vigezo vya sababu…

Kitendo cha kutongoza kina ufundi wake, na wanaume walivyo wajanja (kwa wale wenye uelewa) wana maarifa yao ya kutongoza. Maarifa hayo hutofautiana tegemeana na aina ya mwanamke ambaye wananiya ya kumtongoza. Licha ya kuwa maarifa haya yametofautiana, mwisho wa siku sababu za yeye kutongoza mwanamke huwa mle mle – sababu za msingi hufanana na moja ambayo ni kubwa kuliko zote ni tamaa.

Katika ulimwengu wa utongozaji mambo yamebadilika sasa to the extent hata akina dada/mama huwa tunajilipua once in a while. Ila ukweli unabaki bado kwa kiasi kikubwa wanao ongoza kutongoza ni akina kaka/baba. Na katika kutongoza huko wengi huwa na sababu mbali mbali za kumtongoza huyo mtongozwaji.

Zinazofuata ni sababu hizo zinazomfanya huyo kaka/baba afanye maamuzi na kufanyia kazi malengo yake ya kumpata huyo anae kuwa kadaka jicho lake. Hizi ni sababu tokana na mtazamo wangu ambazo huwa vigezo vya sababu ya kutongoza mwanamke:-

 Anakujaribu

Ni mara nyingi nimesikia kaka/baba zetu wakiweka wazi kukubaliwa na mwanamke aliye mtongoza na kukubaliwa bila kutarajia. Ni kuwa just for the sake of it, mazingira yanakuwa yanaruhusu anajikuta kutongoza kwa kujifurahisha na kujaribu alafu anajikuta mwanamke kakubali. Kama hajajipanga anatahamaki na hata kushindwa kuendeleza azma ya kukutana naye kimwili hasa kwa vinajana ambao hawana makazi badala yake hulelewa na familia hivyo kuwa na sehemu ya kukutania na mwanamke kwa ghafla ni mtihani kwake. Mwingine akikujaribu ukakubali atalala na wewe na hali mwingine atakupotezea na mwanamke akibaki akishangaa inakuwa kakubali na hatafutwi. Continue reading

By ashadii

Wapenzi wa aina hii ni HATARI kwa afya yako…

Kwa mara nyingine nashare yale niliyo nayo katika mahusiano yetu haya ya kila siku ambayo tunafurahia na wakati mwingine kutuendesha.

Ukiwa na mtu (mpenzi au rafiki, mchumba ama mwenza) mara nyingi matarajio huwa ni kufurahi na kufarijika juu ya mwenzi wako ama yale ambayo yahusiana na nyie. Mara nyingi, wengi hutaka kuwa moja ya sifa iwe mtu wake huyo awe sehemu ya maisha yake kuwa na amani na furaha kwa namna moja ama nyingine…

Kama wanadamu kukwazana hakuepukiki na wnegi wanasema ni moja ya kuimarisha mahusiano yenu. La msingi ni kuwa, hata mkikwazana vipi mna uwezo wa kurudi kwenye mstari na kuendelea na mahusiano yenu kama kawaida. Hata hivo wanadamu tumetofautiana na kuna wale ambao waweza kuwa wapenzi ila mmoja wao akawa ni mwenye tabia ya kudhoofisha afya (psychologically, physically hata emotionally) ya mwenzi wake aidha kwa makusudi ama kwa kutojitambua. Mtu wa namna hii akikuta mpenzi wake ni ‘hewalaah!’ kwa kila jambo ndipo ambapo huyo muathirika hugeuka trailer.

Kawaida hawa wapenzi ambao ni hewala maarufu kama ‘Msukule wa Mapenzi’ (in courtesy of ‘Mbu’ wa Jamiiforums) wengi sana huwa hawajitambui. Kwa maana nyingine hata wewe msomaji unaweza kuwa mmoja ya hao watu na bado ukawa hujui. Unaweza jitazama upya kwa kuangalia baadhi ya viashiria hapa chini kupima kama mwenzi wako anaimarisha ama kudhoofisha afya yako. (Zingatia kuwa mara nyingi ni kama huyo mtu ana zaidi ya traits 3/4 ama zaidi ya hizi zilizootedheshwa.)

Continue reading

By ashadii

Umewahi jiuliza upo na Mpenzi/Mwenza wako kwa sababu gani?

Upo na MPENZI/MWENZA wako kwa sababu gani?

Kuna msemo “All is fair in love and war” – ni kwa msemo huu ambao unaweza elewa maana yake – maana ingekuwa kila mmoja ana uwezo wa kusoma akili ya mtu wake kujua yupo nae kwa ajili ipi, nadhani ingekuwa balaa zaidi ya faida. Na hili ni kwako pia msomaji… Are you true to yourself? Umewahi jiuliza honestly upo na mpenzi wako kwa sababu ipi/zipi.

Mapenzi ni mchezo wa ajabu saana. Wanadamu hutaka awe na wa karibu wake hasa Mpenzi kwa sababu tu kuwa anapendwa na anapenda pia. Haijalishi mpenzi huyo ni kitu gani kiliwaunganisha na kuwa wapenzi, iwe ni mapenzi ya dhati juu yake, iwe kwa ajili ya hitaji Fulani toka kwake, iwe kwa sababu ya muonekano wake – mwisho wa siku kwa wale waliopo katika mahusiano ya muda mrefu hujifunza na hatimaye kutambua kuwa mapenzi ni kiungo kimoja wapo tu cha viuongo vingi vya kuwa katika mahusiano na mtu wako huyo. Kuna viungo vingine huwepo na  pengine kuwa hata na nguvu zaidi kuliko hata kiungo cha ‘Penzi’ katika mahusiano hayo.

Mapenzi ni muhimu katika mahusiano, ila bado nafasi yake ni ndogo ukifananisha na viungo vingine. Mahusiano siku zote suala si kuangalia Mapenzi tu sababu pamoja na kuwa mapenzi ni muhimu bado yana nafasi ndogo tu katika kujenga mahusiano thabiti yaliyojaa furaha na amani. Unaweza usiwe umempenda kwa dhati mtu wako ila ukaridhika na kumkubali bila kujalisha yupo vipi ama ni wa hali gani; hilo likafanya kuwa na Amani katika mahusiano yenu alimradi na mtu wako awe hivyo pia.  Kuna watu ambao wapo pamoja na hawana mapenzi yale ya dhati na wana amani na furaha tokana na kuheshimiana, kujaliana na kuthaminiana, na hali hapo hapo kuna wale ambao wana mapenzi ya dhati na mapenzi yao yana matatizo mazito ambayo wanashindwa kabisa kuyaweka sawa kwa wao kuwa na amani katika penzi lao hilo.

Continue reading

By ashadii